Header

‘Nyumba za Yamoto inabidi wazimalizie wenyewe wawe na uchungu’ -Mh.Temba.

Kwenye taarifa njema zilizowahi kutolewa na kundi la Mkubwa na Wanawe ni pamoja na taarifa ya vijana hapo kujengewa nyumba na kituo hicho ambapo nyumba hizo tulifahamishwa kuwa nyumba hizo ziko Mbande Kisewe jijini Dar es salaam,taatifa hii wakati inatoka ilikuwa ni Nov 2016.

Sasa hivi ni zaidi ya miezi 3 toka nyumba hizo zitambulishwe na Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe Said Fella na kusema kuwa hakuna muda mrefu wasanii hao watakua wamehamia,XXL ya Clouds FM imempata mmoja kati ya viongozi wa kundi hilo Mh Temba ambaye kakubali kuelezea usahihi wa taarifa za nyumba hizo.

Mheshimiwa Temba>>’Nilishaongea na Management wenzangu nikawaambia hawa sasa hivi inabidi wajitegemee wenyewe hata hizi pesa zao wenyewe hatutaki kuzishika sasa hivi tunatakiwa kuweka mezani tuwaambie hiki na hiki kwa sababu washakua watu wazima kama mtu unaweza kumpa Milion 5 anaamua kwenda kula bata atajijua mwenyewe’

‘Zile nyumba nishamwambia Boss vitu vingine wanatakiwa kumalizia ili wajue uchungu wa kuhangaika kwenda kununua tiles,kwenda kununua umeme,kufanya hivi na hivi kwa sababu hata sisi tumehamia kwenye nyumba zetu hazina maji hazina umeme,inatakiwa wahamie sasa hivi wajue tunalala vipi kwenye joto,nyumba hazikamilika kiukweli lakini mtu kuishi kama kuishi unaweza,ili tiles,maji na umeme ndio bado’ -Mheshimiwa Temba.

Comments

comments

You may also like ...