Header

Baada ya Marekani Ali Kiba kuelekea London

Msanii wa Bongo Fleva Ali Kiba  ambae anafanya vizuri kwa sasa kupitia wimbo wake wa Aje amepata nafasi ya kushiriki katika tamasha kubwa la mitindo huko london

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ali Kiba amewajuza mashabiki zake kwa kupost ujumbe  ulioonesha kupata nafasi ya kutumbuiza katika tamasha hilo ambalo linafahamika kama One Africa Premium Fashion litakalofanyika tarehe 12 mwezi wa 5  Jijini London akiwa na wasanii wengine kama Victoria Kimani ,Flavour,Bank W ,Tiwa Savage na wengine “One Africa Fashion at the heart of London Cc @pauloo2104 #alikibaworldtour2k17 #kingkiba”

Ali kiba bado yuko nchini Marekani ambapo anaendelea na tour yake  akiwa pamoja na ndugu yake Abdu kiba

Comments

comments

You may also like ...