Header

Ray Kigosi achoshwa na Watanzania; Amfananisha Kanumba na Diamond Platnumz

Muigizaji wa filamu nchini Tanzania Ray ameamua kuwachana watanzania ambao hawana jambo la kufanya zaidi ya kuwakatisha tamaa wale watu wanaojituma kwenye kazi zao badala ya kuwafariji na kuwashauri .

Ray akitolea mfano wa Marehemu Steven Kanumba na Diamond Platnumz amesema awali Kanumba alishawahi kukatishwa tamaa na watanzania kwa kuambiwa kuwa ni Freemanson na wengine kumtabiria kuwa hatafika mbali kwenye sanaa yake lakini leo anashangaa wale wale watanzania waliokuwa wanamponda ndiyo hao wanaomsifia leo kuwa haitatokea muigizaji mkali kama Kanumba.

“1.Kanumba alipoanza kuona mwanga wa kufanikiwa bila kujali juhudi zake kuna watu walimuita Freemanson, Mara anatumia nguvu za Giza. that is to say films zake hazikuwa nzuri but ziliuza sababu ya nguvu za Freemanson na nguvu za giza !!,2.Kanumba alipoenda Big Brother alipondwa Sana na kuitwa bogus kwa Madai hajui kiingereza, Ni watanzania Hawa Hawa walibebea bango hili huku baadhi ya waandishi uchwara wakieneza ujinga huu bila kujali juhudi zake. But Leo wanamsifia hakuna Kama Kanumba !,3.Kuna wakati Kanumba alionekana wazi kuvunjwa moyo na kukatishwa tamaa kwa kuonekana juhudi zake si kitu. But Alisema maneno machache Kuwa mtanikumbuka kama si Leo basi Ni Kesho,and alichosema kimetimia, wale wale waliokuwa wakisema Ni Freemanson bila hata kujali juhudi zake kwenye game Leo ndio kwa unafiki wanasema hakuna Kama Kanumba”.Ameandika Ray Vicent Kigosi kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Ray aliendelea kutoa mifano na kwenda mbali zaidi zaidi kwa kumfananisha Kanumba na Diamond Platnumz kwa kusema hata Diamond pia kuna kipindi baadhi ya watanzania na waandishi wa habari walikuwa wanamwambia ni Freemanson hata mganga wao wanamjua na ilifikia pahala walimtabiria kuwa atadondoka kwenye muziki lakini yeye hakujali aliendelea kupiga kazi na tumeona kila kukicha anazidi kupanda juu.

Diamond Platnumz nae baada ya kuona Njia ya mafanikio kuna watanzania, wasanii wenzake na hata baadhi ya wanahabari wanasema Ni Freemanson, wengine wanaonyesha chuki ya wazi kwake. Wanasema Hana muziki mzuri, Mara Ni Kiki tu ambazo hata Kanumba alikuwa akiripotiwa magazetini na kina Wema .
Hawaoni juhudi na thamani ya Diamond sasa ! Hatuombi baya limpate Diamond ili kudhibitisha tabia na unafiki wa binadamu. But HAO NDIO BINADAMU siku zote hawana Jema unafiki ni sehemu ya Maisha.”Aliendelea kuandika kwa kusema
Kila siku Ni kuzua hii na kile, Mara ooh Diamond Ni mchawi, kasema mleteni huyo mganga wangu mkashindwa kumleta, akajitokeza mganga fake sijui na Madai juu Kuwa Diamond atashuka kimuziki kwasababu ananipuuza niliyempa nyota, Diamond akasema sawa namtegemea Mungu. Miaka 4 sasa tangu yaliyoitwa ya mganga Diamond hashuki ndio anazidi kupaa. HAO NDIO BINADAMU kusema lolote Ni haki Yao.“Ameandika Ray kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Amemaliza kwa kusema watanzania tuwe wepesi wa kuvipa vitu vyetu dhamani kwanza hata japo kidogo kwani leo hii kanumba aliyekuwa anaonekana hajui Kiingereza na Filamu zake mbovu leo inaonekana filamu zake ni bora sana wakati walimbeza hao hao watanzania.

Kazi za Kanumba sasa zinapewa thamani na ubora uliovuka mipaka na viwango ambao hakupewa kipindi yupo hai ! HAO NDIO BINADAMU na tabia zao
Ni tabia tu ya baadhi ya watu kubebea mabango mabaya ya Mtu au uzushi na kuacha mazuri yake then baadaye wakishikwa Uchawi wanageuza walichoamini Ni nyeusi kiwe nyeupe !!
Tukosoe penye tija na tutoe appreciation“Amemaliza kwa kuandika hivyo.

Comments

comments

You may also like ...