Header

Leo ni vita ya Bailly na Aguero kwenye Jiji la Manchester

Beki  wa kati wa Ivory Cost Eric Bailly amekuwa na mwanzo mzuri tangu aanze kucheza Manchester United kufuatia uhamisho wake wa paundi milioni 30 akitokea Villarreal majira ya joto msimu uliopita.

Bailly alipata majeraha lakini ameendelea kucheza katika kiwango chake cha juu bila kujali wapinzani wake ni akina nani.akicheza pamoja na Marcos Rojo, Bailly amekuwa na kiwango cha hali ya juu zaidi, lakini kuumia kwa Mwargentina huyo wiki iliyopita kumemlazima Bailly kushirikiana na Daley Blind dhidi ya Burnley.

Bally leo atakuwa na kazi ya kumzuia Mwargentina Sergio Aguero ambaye amefunga mabao 30 kwenye michuano yote msimu huu, 17 kati ya hayo yakitoka kwenye ligi

Mshambulizi huyo ametengeneza nafasi 22 kwenye ligi, kwa hiyo anahitaji kudhibitiwa vikali sawa na washambulizi wengine kwenye timu.

Comments

comments

You may also like ...