Header

Mwambusi awapa onyo kali Mbao FC

Kocha msaidizi Yanga, Juma Mwambusi ameitaka Mbao FC kujiandaa na kipigo hasa baada ya mshambuliaji wao wakimataifa kutoka Burundi Amissi Tambwe kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.

Akizungumza na DizzimOnline Mwambusi amesema uwepo wa Tambwe unawapa matumaini makubwa kutokana na uwezo wa mshambuliaji huyo wa kufunga mabao anapokuwa uwanjani.

Mbao tunawaheshimu lakini wanajua Yanga tunakwenda na hatutakuwa na mzaha tunapokuwa kwenye eneo lao la goli tunaye Tambwe wenyewe wanamjua pia yupo Chirwa kwahiyo wajiandae kwa kipigo,” amesema Mwambusi.

Yanga na Mbao wataumana jumapili kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho FA kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.

Comments

comments

You may also like ...