Header

Simba yahaidi kuitafuna Azam FC

Simba  imeapa kufa na Azam baada ya kuona njia pekee itakayowasaidia kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao ni kunyakua taji la Kombe la FA,Wekundu wa Msimbazi  imeingia hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho kwa kuitoa Madini FC ya mkoani Arusha.

Akiongelea maandalizi hayo mkoani Morogoro walipojificha kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo, kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, alisema wanajiandaa vya kutosha kuhakikisha wanasonga mbele kwenye mchezo huo.

“Mechi itakuwa ngumu ila kwa hali ilivyo kwa sasa hasa kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara japo bado tupo kwenye mbio za ubingwa, lakini ili tujihakikishie nafasi ya michuano ya kimataifa ni kuchukua Kombe la FA. Alisema Mayanja.

Wekundu hao wa Msimbazi wanajua kile wanachopaswa kufanya dhidi ya Azam kwani kupoteza mchezo huo itakuwa wameondolewa moja kwa moja kwenye ndoto zao za kushiriki michuano ya kimataifa hapo mwakani kwa kuwa kwenye ligi tayari Yanga wana nafasi kubwa ya kutetea taji lao

Comments

comments

You may also like ...