Header

Coman apata shavu la kuendelea kuitumikia Bayern Munich

Bayern Munich imethibitisha usajili wa Kingsley Coman kwa mkataba wa kudumu kutoka Juventus mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekuwa akitumika kwa mkopo Bayern tangu mwanzo wa kampeni za 2015-16, akiwa na umri wa miaka 20 na kucheza mechi 35 msimu wake wa kwanza Allianz Arena.

Coman amefunga mara mbili tu katika mechi 17 Bundesliga msimu huu, na imedaiwa kuwa Bayern hawakuwa na mpango wa kubaki na mchezaji huyo aliyekuwa akihusishwa na tetesi za kujiunga na Arsenal na Chelsea.

Mkurugenzi mtendaji wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge amesema: “Ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa. Tumeshawishika kwamba atakuwa na msaada mkubwa miaka ijayo.”

Coman amecheza mechi sita kwenye timu ya taifa ya Ufaransa kwenye michuano ya Ulaya 2016

Comments

comments

You may also like ...