Header

AY apata nafasi ya kusikiliza wimbo mpya wa Darassa

Msanii na mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Ambwene Yessaya a.k.a AY amemsindikiza hitmaker wa wimbo unaokwenda kwa jina ‘Muziki’ Darassa katika show kubwa iliyopewa jina la ‘B-club Pool Party’ itakayofanyika tarehe 30 April siku ya jumapili mjini Nairobi nchini Kenya.

Akizungumzia ukaribu na kilichompelekea kumsindikiza Darassa katika safari ya show yake nchini Kenya, AY amesema kuwa imekuwa ni kazi ya muda mrefu katika ushiriki na wakongwe wenzake katika muziki kuhakikisha wanaiunganisha Afrika mashariki kimuziki kiasi cha kufanikiwa kwa kiasi kikubwa katika hilo hata kuweza kujivunia zao la baadhi ya wasanii wapya wanaofanya vizuri ambapo hakusita kuuzungumzia ujio wa ngoma nyingine ya Darassa kwa kusema kuwa ni ngoma kali sana kutokana na uzoefu wa sikio lake alionao kama msanii hivyo wiki ijayo mashabiki wakae tayari.

“Darassa bado ana kazi nyingine nimeisikiliza ni nzuri sana…yaani ni next wiki tu itatoka” Alisema AY alipokuwa akizungumza na The Trend ya NTV.

Hata hivyo onesho hilo litakalofanyika katika kiwanja cha kujirusha cha B-Club kilichopo Parklands mjini Nairobi, Kenya Darassa atasindikizwa na mshiriki na aliyeimba chorus na bridge ya wimbo wa ngoma ya ‘Muziki’ Ben Pol.

Comments

comments

You may also like ...