Header

​OFFICIAL: Tottenham Hotspur yahamia Wembley 

Klabu ya Tottenham hotspurs imethibitisha kuutumia uwanja wa Taifa wa England, Wembley kama uwanja wao wa nyumbani kwa michezo yao yote kwa msimu ujao 2017/2018,  Kufuatia ujenzi wa uwanja wao mpya.

Spurs ambao wametumia uwanja huo msimu huu kwa baadhi ya michezo ya UEFA pamoja na ile ya Europa ligi wamethibitisha kuendelea kuutumia uwanja wa Wembley kama uwanja wao wa nyumbani kwa msimu ujao, kupitia website ya klabu hiyo baada ya kukubaliana na chama cha soka nchini Uingereza, FA.
Klabu hiyo imeanza ujenzi wa uwanja mpya pembeni ya uwanja wao wa White Hart Lane utakaowagharimu kiasi cha £750 Millioni.
Spurs ambao wapo nyuma kwa alama nne mbele ya vinara Chelsea katika ligi kuu nchini Uingereza watacheza mchezo wao wa mwisho katika uwanja huo wa White Hart Lane msimu huu dhidi ya Manchester united tarehe 14 mwezi wa tano.

Comments

comments

You may also like ...