Header

Bao moja la Mbao FC laizimisha Yanga

Klabu ya Soka ya Mbao FC inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara imetinga hatua ya Fainali ya Michuano ya Azam Sports Federation Cup baada ya kuifunga Klabu ya Yanga bao moja kwa Sifuri katika Dimba la CCM kirumba jijini Mwanza.

 Mbao FC ambao walikua wenyeji katika Mchezo huo walipata Goli mnamo dakika ya 26′ Ya mchezo baada ya Beki wa Yanga Andrew Vicent “Dante”  kujifunga kwa kuunganisha Krosi iliyopigwa na mchezaji Pius Buswita Wa Mbao FC. 

Mbao FC inaungana na Klabu ya Soka ya Simba katika hatua ya Fainali, Simba ilishinda Mchezo dhidi ya Azam Fc hapo Jana. 
Hii ni Mara ya Kwanza kwa Klabu ya Mbao Fc kutinga hatua ya Fainali ya Kombe hili tangu Lilipoanzishwa kwa Mara ya Pili Mwaka jana. 
Mshindi wa Michuano hii atapata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika Michuano ya kimataifa ya kombe la shirikisho kwa ngazi ya vilabu.

Comments

comments

You may also like ...