Header

Bayern Munich watwaa ubingwa wa Bundesliga

Baada ya Ushindi wa Jana wa bao 6  dhidi ya Wolfsburg katika dimba la Volkswagen Arena, Klabu ya soka ya Bayern Munich “The Bavarians” Imetangazwa kuwa Mabingwa wa Ligi kuu nchini Ujerumani. 

Klabu hiyo imenyakua Ubingwa baada ya kucheza Jumla ya Michezo 31 Wakiwa kileleni kwa Jumla ya Alama 73 mbele ya Leipzig ambao wana alama 63 huku kukiwa kumesalia Michezo Mitatu kabla ya Ligi hiyo kumalizika. 
Bayern Munich inakua klabu ya kwanza kutwaa ubingwa wa Bundesliga mara tano Mfululizo baada ya kutwaa ubingwa huo kuanzia msimu wa mwaka 2012/2013 mpaka Msimu huu wa mwaka  2016/2017 huku ukiwa ni ubingwa wao wa 27 Tangu klabu hiyo ipande Ligi kuu.

Comments

comments

You may also like ...