Header

“Hatumuogopi Yanga wala Mbao FC” -Jackson Mayanja

Baada ya Wekundu wa Msimbazi kufanikiwa kutinga fainali ya Kombe la FA kocha msaidizi wa timu hiyo Jackson Mayanja amesema wapo tayari kukutana na timu yoyote fainali kutokana na ubora wa kikosi chao.

Mayanja raia wa Uganda amesema hayo mbele ya Wandishi wa Habari baada ya mchezo kumalizika  kuwa kiwango walichokuwa nacho Simba kwasasa kinawaruhusu kucheza na timu yoyote Afrika hivyo kama wataingia fainali wapinzani wao Yang au Mbao FC wapo tayari kukabiliana nao.

Kila mtu ameshuhudia kiwango chetu hatukushinda kwa kubahatisha tulipambana na kuonyesha ujuzi wetu ndiyo sababu ya kutinga fainali, hatuihofii Yanga wala Mbao sababu ni timu za kawaida ukilinganisha na sisi,”Alisema Mayanja

Nusu fainali nyingine ya kombe la FA kati ya Mbao na Yanga inachezwa leo uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na mshindi atacheza na Simba kwenye tarege ambayo itatangazwa na Shirikisho la soka Tanzania

 

Comments

comments

You may also like ...