Header

Idris Sultan agundua tatizo kubwa la kuanguka kwa tasnia Tanzania

Muigizaji na mchekeshaji kutoka Tanzania anayendelea kufanya vizuri kupitia filamu ya ‘Kiumeni’ kama Gasper ‘Idris Sultan’ amezungumzia kikubwa kinacholeta changamoto ya kudolola kwa kiwanda cha burudani Tanzania.

Akizungumzia matabaka yaliyopo katika burudani Tanzania, Idris amesema kuwa tatizo kubwa ni ushabiki uliopitiliza kiasi cha kuzalisha chuki kati ya waliojitokeza kuleta mabadiliko chanya katika tasnia ya burudani kwa kufanya mambo tofauti tofauti.

“vijana wa bongo wanazidisha ushabiki, ushabiki ambao hauna maendeleo to some level ambayo kama mimi namkubali Tambwe sina sababu ya kumbubali Idris…badala ya kumkubali Tambwe ili afike mbali nitakazana katika kumtukana Idris. Kitu ambacho sio kizuri yaani ni ushabiki ambao ni kama tunadhohofishana” Alisema Idris kupitia The Playlist ya Times Fm.

Hata hivyo Idris mwenye kiwango kikubwa cha umaarufu Afrika amewasisitiza watanzania kukubali uwepo wa wawakilishi wengi wenye dhamana ya kuiwakilisha Tanzania kivyovyote ili kukuza tasnia na heshima ya taifa la Tanzania kwakuwa hata nchi zilizokua zaidi hasa kiburudani zina watu wengi tofauti na wenye umaarufu wa kiwango cha hali ya juu huku akitolea mfano idadi kubwa ya wasanii na watu maarufu kutoka Marekani.

Comments

comments

You may also like ...