Header

Kuelekea mchezo wa Mbao FC vs Yanga: Mkwasa alia na Mashabiki

Katibu mkuu wa Klabu ya soka ya Yanga, Charles Boniface MKwasa amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi katika Pambano lao dhidi Klabu ya soka ya Mbao Fc katika mchezo wa nusu Fainali ya michuano ya Azam Sports Federeation Cup ili kuipa nguvu timu hiyo kuibuka na ushindi.

Kikosi hicho cha Yanga chenye wachezaji 22 pamoja na Viongozi 8, kiliwasili Jijini Mwanza Siku ya Alhamisi tayari kwa  Mchezo dhidi ya mwenyeji wake Mbao Fc katika uwanja wa CCM Kirumba jijini mwanza siku ya Jumapili katika nusu Fainali ya Pili ya Michuano hiyo.

Mashabiki hasa wa mikoa ya jirani na Mwanza kama vile Musoma, Shinyanga, Mara na maeneo mengine ya jirani wajitokeze kwa wingi ili kuisapoti timu yao maana naamini mechi itakua ngumu na hatuwezi idharau timu ya mbao kwani imeleta ushindani mkubwa mpaka kufikia hatua ya nusu fainali” Alisema Mkwasa kwenye mahojiano yake na Dizzim Online. 
Kuelekea mchezo huo leo jioni Klabu ya Yanga imethibitisha kuwakosa baadhi ya wachezaji wao wa kikosi cha kwanza kutokana na sababu mbalimbali akiwemo Malimi Busungu, Vicent Bossou pamoja na kiungo Donald Ngoma.

Comments

comments

You may also like ...