Header

Sunderland bye! bye! EPL

Timu ya Ligi kuu England, Sunderland imeshuka daraja rasmi baada ya mfululizo wa matokeo mabaya na jana kuruhusu kipigo cha goli moja dhidi ya Bournemouth ,Goli lililowaonesha njia ya kutokea.

Sunderland ambao wameshuka kwa mara nne kwenye misimu tofauti tofauti ya EPL,walikuwa uwanjani kwao Stadium of Light wakati wakiikaribisha timu ya Bournemouth na mashabiki wao waliamini wanaweza pata matokeo katika mchezo huo lakini wapi bahati haikuwa kwao kwani Joshua King mnamo Dk ya 88 alipachikia Goli Bournemouth goli  lililodumu mpaka filimbi ya mwisho.

Baada ya mchezo huo, kocha wa Sunderland David Moyes alisema hana mpango wa kuondoka katika klabu hiyo bali anataka kupambana ili kuirudisha tena ligi kuu.

“Klabu yangu (Sunderland) itapambana tena kurudi ligi kuu na naamini hilo nawaahidi mashabiki msimu ujao tutarudi tena“Alisema Moyes baada ya mchezo.

Comments

comments

You may also like ...