Header

Himid Mao kwenda kujaribu maisha mapya Ulaya

Kiungo wa Azam FC  na timu ya taifa ya Tanzania Himid Mao ameondoka nchini Mei 1, 2017 kuelekea Denmark kwa ajili ya majaribio ya kutafuta kucheza soka la kulipwa barani Ulaya anakwenda kwenye klabu ya Randers FC inayoshiriki ligi kuu nchini humo ligi inayojulikana kwa jina la Superliga.

Kwa mujibu wa kwa Shaffi Dauda Himid alisema kabla ya kuondoka: “Naenda kwenye klabu ya Randers FC ya nchini Denmark kwa ajili ya majaribio kwa muda wa siku 15, kama mchezaji najiamini naweza kufanya lolote sehemu yoyote, mambo mengine ya mbele anajua Mungu,” amesema Himid muda mfupi kabla ya kuondoka ardhi ya Bongo.

Mimi wajibu wangu ni kujitolea kadiri niwezavyo na kuwashawishi hao kwa uwezo wangu wote patakapobakia ni kazi ya Mungu”

Kiungo huyo ameonesha kiwango cha juu katika msimu huu kuanzia kwenye mechi za ligi kuu Tanzania bara, kombe la Azam Sports Federation Cup, michuano ya kimataifa pamoja na mechi za timu ya taifa

Comments

comments

You may also like ...