Header

Kuwatoa Yanga kumeniletea heshima nyumbani Burundi ” Ettiene”

Kocha wa Wababe wa Yanga, Mbao FC  raia wa Burundi Ettiene Ndayiragije, amesema anajiona mtu muhimu kwenye timu hiyo baada ya kuifunga  na kuwavua ubingwa wa Kombe la FA.

Kocha huyo aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza kwa kufuata kile alichowaelekeza mazoezini hata kupata ushindi huo ambao umemfanya hata kurudisha heshima kwao Burundi .

Nilipanga kufanya maajabu na nafurahi kuona yametimia hii imeniletea heshima hata nyumbani Burundi ambako nilikuwa naonekana kocha wa kawaida lakini leo kuitoa timu kubwa ya Yanga ambao ndio mabingwa watetezi kumelipaisha juu jina langu,” amesema Ndaliyagije

Ettien amsemaAhawezi kuwazungumzia wapinzani wao Simba kwa sababu hajajua tarehe ambayo watacheza mechi ya fainali lakini kitu cha muhimu wataendelea kujipanga ili kuhakikisha wana shinda mchezo huo.

Comments

comments

You may also like ...