Header

Simba yaanza mandalizi kwa ajili ya Msimu ujao

Wekundu wa Msimbazi Simba wametinga fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania na kufufua matumaini ya kuweza kushiriki michuano ya kimataifa mwakani, sasa wameanza kusuka upya kikosi chao.

Simba wametinga fainali kwa kuichapa Azam fc kwa bao 1 kwa 0 huku Mo Ibrahimu akiwa shujaa kwa upande wa Mnyama kwenye Dimba la Taifa  jijini Dar es Salaam kwa kutinga fainali wameanza kwakuiitaji saini ya beki wa Toto Africa Yussuph Mpilili.

Akiznungumza na Bingwa Mpili amesema kuwa “Simba wameonyesha nia ya kutaka kunisajili kwa ajili ya msimu ujao na tayari tumeanza mazungumzo ili kukamilisha mpango wa kumuitaji kikosini kwao”

Tetesi zinasema kuwa baadhi ya klabu nyingine zinamtaka  beki huyo ni Yanga Azam na Singida United.

Comments

comments

You may also like ...