Header

Hawa ndo wasanii wanaotarajia kuachia ngoma muda wowote kuanzia sasa

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania wanaoendelea kufanya vizuri huku wengine wakiendelea kuingia kwenye mzunguko wa uchezaji wa nyimbo kwa ngoma mpya. Mbali na Young D na wengine kuachia ngoma basi wafuatao ni wasanii wengine watakao achia mwishoni mwa wiki wiki hii na wiki ijayo.

  1. Nedy Music.

Wimbo wa mwisho:Rudi.

Alishirikiana  na mkali wa melody na sauti Christian Bella chini ya utayarishaji wa Abbydady.

 

  1. Darassa.

Wimbo wa mwisho: Muziki.

Ni wimbo aliyomshirikisha Ben Pol uliondaliwa na watayarishaji watatu ambao ni Mr. Vs, Abbah na Mr T Touch.

  1. Stamina.

Wimbo wa mwisho: Nitampigia.

Stamina alimshirikisha Mr. Blue ikiwa wazo la wimbo huo lilitolewa na rapa Baghdad.

  1. Dogo Janja.

Wimbo wake wa mwisho: Kidebe.

Ni wimbo uliotoka mwishoni mwa mwaka jana chini ya utayarishaji wa Daxo Chali katika studio za MJ Records.

Aidha wapenzi wa muziki mzuri wanahitaji kuwa tayari kupokea kazi za wasanii hawa kwakuwa siku zote wamekuwa ni wasanii wanaofanya kazi ambazo zinavigezo vya kuitwa muziki mzuri.

Comments

comments

You may also like ...