Header

Janet Jackson kuanza tena ziara yake ya muziki baada ya kujifungua

Janet Jackson ametumia Twitter usiku wa Jumatatu kutoa matangazo muhimu kuhusu familia yake pamoja na kuirudisha tena ziara yake ya muziki. Janet ametumia video ya dakika moja na nusu kuelezea kunenepa kwake pamoja na mwanae mwenye miezi mitatu sasa, Eissa Al Mana ambaye hivi karibuni alimuonesha kwenye mitandao ya kijamii.

“Hey you guys, it’s me Jan, just in case you didn’t recognize me cause I have put on quite a few since I had the baby,” anasema Jackson. “I thank God for him, you guys. He’s so healthy, so beautiful, so sweet, so loving, such a happy baby.”

Kwenye video hiyo pia amezungumzia kuachana na mume wake bilionea, Wissam Al Mana, akidai kuwa ametaka kuwa mkweli kwa mashabiki wake. “Yes, I separated from my husband. We are in court and the rest is in God’s hands,” amesema.

Ametangaza pia atairejesha ziara yake ya Unbreakable ambayo ameibadilisha jina kuwa ” “State of the World” tour. “It’s not about politics” ameelezea kubadilisha kwa jina la ziara yake. “It’s about people, the world, relationships and just love.”

Jackson aliahirisha ziara hiyo mwanzoni mwaka 2015 ili kufanyiwa upasuaji na tena akaisitisha April 2016 baada ya kutangaza kuwa yeye na mumewe wamepanga kuwa na familia.

Ziara yake hiyo itaanza rasmi September 7 huko Lafayette, Louisiana.

Comments

comments

You may also like ...