Header

Mtoto wa Michael Jackson, Paris ala shavu la kuwa kisura wa Calvin Klein

Binti wa hayati Michael Jackson, Paris Jackson amekula shavu la ‘seven figure.’
Mtoto huyo wa MJ na Debbie Rowe ameripotiwa kuchaguliwa kuwa kisura wa is Calvin Klein.

Mrembo huyo ametokea kujipatia umaarufu kwenye ulimwengu wa fashion. Kwa sasa amesainishwa na kampuni ya urembo ya IMG Models, ambayo inawasimamia pia warembo kama Gigi na Bella Hadid, Hailey Baldwin na Ashley Graham. Pia ameshaonekana kwenye majarida ya Rolling Stone, Harper’s Bazaar na CR Fashion Book.

Taarifa hiyo imekuja baada ya kuripotiwa kuwa Paris pia amepata shavu la kuigiza kwenye filamu kwa mara ya kwanza. Baada ya tangazo hilo Paris alitweet, “i love how stoked everyone is about this but honestly it’s just one scene it’s not like i have my own feature film lol.”

Comments

comments

You may also like ...