Header

Kanye West ajiondoa Twitter na Instagram

Kanye West hana tena mpango na mitandao ya kijamii. Rapper huyo amejiondoa Twitter na Instagram kwa wakati mmoja kuanzia Ijumaa hii.

Haijulikani kwanini Yeezy ameamua kufuta akaunti zake, hata hivyo amefanya hivyo kabla ya kuzindua nguo zake za watoto alizozibuni na mkewe Kim Kardashian.

Kanye ameendelea kujitenga na macho ya umma siku za hivi karibuni. Wiki iliyopita hakutokea kwenye hafla ya Met Gala iliyohudhuriwa na mastaa kibao akiwemo mkewe.

Comments

comments

You may also like ...