Header

Simtaki Trump kwenye show yangu – Ellen DeGeneres

Rais wa zamani wa Marekani, Barack na mkewe Michelle, walikuwa wageni wa mara kwa mara kwenye kipindi cha Ellen DeGeneres. Lakini, usitegemee siku moja kumuona Rais wa sasa, Donald Trump akihojiwa kwenye The Ellen DeGeneres Show.

Akizungumza na Matt Lauer kwenye kipindi cha Today cha NBC, Ellen alisema hawezi kumwalika Trump kwenye show yake. Akitaja sababu ya kufanya hivyo, Ellen alisema, “Sababu siwezi kubadilisha mawazo yake. Anapinga kila kitu ninachokisimamia. Tunahitaji kumuangalia mtu mwingine ambaye hafanani na sisi na anayeamini katika kitu ambacho sisi hatuamini lakini bado atawakubali na kuwaacha wapate haki zao.”

DeGeneres yupo kwenye ndoa ya jinsia moja, kitu ambacho serikali ya Trump haikiungi mkono.

Comments

comments

You may also like ...