Header

Young D atoboa siri ya tattoo yake ya mwisho

Rapa kutoka Tanzania na hitmaker wa ngoma Bongo Bahati Mbaya(BBM) Young D ametoa sababu za tattoo yake ya mwisho pindi atakapo amua kufanya maamuzi ya kuchora yake ya mwisho ya kumi na moja.

Akizungumzia idadi ya Tatoo kumi alizonazo mwilini Young D amesema kuwa atakapoongeza atachora tattoo ya mwane anayekwenda kwa jina la Tamali kama heshima kwake.

“nina tattoo kama kumi hivi, na bado moja ambayo nahisi nitafungia mwili ya Tamal ambayo bado sijafikiria nitaichora lini au wapi lakini bado nina plan” Alisema Young D kupitia The Playlist ya Times Fm.

Hata hivyo Young D kazi yake ya Bongo Bahati Mbaya imekuwa kazi ya kwanza tangu ilipofahamika kuwa ameachana na uongozi wake wa lebo ya muziki ya MDB na kuanza kufanya kazi chini ya Studio za Touch Sound na mtayarishaji Mr. T Touch.

Comments

comments

You may also like ...