Header

QBoy Msafi ajitahidi kutolea maelezo ya nini kilimtoa machozi

Msanii na hitmaker wa ngoma ya ‘Karorero’ QBoy Msafi ametolea maelezo kilichomfanya atoe machozi mbele ya kamera kwa uchungu mapka kushindwa kuongea baadhi ya mambo.

Akionekana ni mwenye kuyakumbuka mengi kuhusu kupitia maisha ya changamoto QBoy amesema kuwa inasikitisha sana kupoteza muelekeo na chanzo kiwe ni yule uliye muamini hata kuonyesha kuwa kipo kinachochangia kuwa alipo sasa.

“mimi nafikiri kwamba wao wangeelewa kwamba(huku machozi yakimtiririka hata kushindwa kuendelea kuongea) kila mwanadamu ana malengo ya future alafu nina imani kila kijana anazo njia za kumfikisha kwenye malengo…kinachonisikitisha ni kwamba unapopoteza future bado kijana kuwezi kuipata ukisha zeeka.

“unaona kwamba mbona mi nafight ili nifike kwenye malengo alafu anatokea mtu tu anakutoa kwenye malengo ambayo wewe ulikuwa unafight labda huwezi kujua mwanzo ulipokuwa una fight ilikuwa ni ahadi tu za kawaida za kuonyesha kwamba tufanye kazi kesho ipo…yaani wewe unafanya kazi kwa kutegemea kuwa kesho yako inakuwa njema” Alisema QBoy alipokuwa akizungumza na Global Tv.

Hata hivyo QBoy ameonesha wazi kuumizwa sana na tukio lililompotezea muda na baadhi ya malengo hata kuhaidi kufanya makubwa ili kuziba pengo la kilichotokea.

Comments

comments

You may also like ...