Header

Edu Boy aliitamani na kushawishi Chorus ya Mazoea itumike kwenye wimbo wake

Rapa kutoka Tanzania anayefanya vyema na ngoma ‘Naiee’ aliyomshirikisha Bill Nass ‘Edu Boy’ amezungumzia utata na alivyoangaika kupata Chorus ya wimbo wa ngoma yake mpaka kumshirikisha Bill Nas.

Akizungumzia kitendo cha producer Mona Gansta kuikataa Chorus yake licha ya kurecord mara kadhaa Edu Boy amesema kuwa matamanio yake yalikuwa ni kumshwishi Bill Nas ampatie Chorus yake aliyoitumia katika wimbo wa Mazoea aliyomshirikisha Mwana FA.

“nilivyoenda kwa Mona kurecord ile Chorus siku ya kwanza, Mona kaikataa…nilivyorecord siku ya pili Mona kaikataa…nilirecord siku ya tatu Mona akaikata…nikasema sasa kama unaikataa Chorus tutafanyaje?…akasema ukifanya na Bill Nas ikakuwa Chemistry kali sana. Tena Bill Nas nilimuomba anifanyie Chorus ya Mazoea…nikamfata Bill Nas nikamwambia ebwanee naomba unifanyie ile Chorus ya Mazoea uihamishie humu kwasababu ile ngoma alikuwa hajaiachia akaniambia hamna bana Edu Boy naweza kufanya kikubwa zaidi ya kile endapo utaniamini” Alisema Edu Boy alipokuwa akiongea na The Playlist ya Times Fm.

Hata hivyo wimbo huo wa Edu Boy umeonekana kufanya vizuri zaidi ya wengi walivyodhani kupitia video kali ya wimbo iliyoandaliwa na kupendezeshwa na muongozaji wa video za muziki Tanzania Nisher.

Comments

comments

You may also like ...