Header

Karrueche Tran na timu yake wanataka kuniharibia maisha yangu – Chris Brown

Karrueche Tran anatarajia kutoa ushahidi mahakamani kuhusiana vitendo vya unyanyasaji anaodai alikuwa akifanyiwa na ex wake Chris Brown ili kupewa kibali cha kutosogelewa naye milele.
Brown amefunguka kwa urefu kuhusiana na sakata hilo kwa kucomment kwenye ukurasa wa Instagram wa Baller Alert na kukanusha tetesi hizo.

“Nimechoshwa na hawa watu wazima wenye tamaa. Timu yake inajaribu kila wawezalo. Kwanini? Hakuna aliyeniletea makaratasi ya mahakama na kwa umbali wanaoenda, natakiwa kuwaita stalkers. Kinachoudhi zaidi, wamebadilisha mambo ya zamani kwa kusema nilimnyanyasa. Acheni hizo, kufungua majeraha mapya ili kumfanya Kae mhanga, hayo ni mambo maovu. Kinachosikitisha nanyi mnaamini. Mwacheni. Mnanichokoza nipaniki ili mpate kitu. Gundua upuuzi huu hutokea wanapohitaji kupromote kitu. Hakuna anayejali, hasa mimi. Ndio maana nachafuliwa. Hakuna anayewajali kama jina langu lisipohusishwa,” ameandika.

Ameongeza, “Sina shida naye. Unadhani nataka kumfukuzia au kuwa na mtu ambaye anataka kuniangamiza? Hahitaji kibali cha mimi kukaa mbali naye. Mimi ndio nahitaji dhidi yao.
Na sitokubali tu makaratasi kutoka kwa mwanasheria yeyote na sitoenda mahakamani kukubali kuwa nina hatia kujiharibia zaidi nilivyo. Sikupatikana na hatia kwenye kesi ya Rihanna kwasababu sikuwa na hatia. Nakataa kuwaruhusu watu hawa wenye mioyo ya kishetani kunibandika na kudanganya kwasababu wanadhani itapandisha juu career zao. Kaeni mbali na mimi.’

Comments

comments

You may also like ...