Header

Msanii wa lebo ya Don Jazzy amshirikisha Vanessa Mdee

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Nigeria anayefanya kazi chini ya usimamizi wa records lebo ya ‘Marvin Records’ inayomilikiwa na mkali aliyetajwa katika orodha ya wasanii 10 tajiri Afrika ‘Don Jazzy’ muite Reekado Banks ameachia ngoma aliyomshirikisha msanii kutoka Tanzania Vanessa Mdee.

Mapema leo Reekado Banks ameachia rasmi video ya wimbo unaokwendwa kwa jina ‘Move’  unaotajwa kuwa wimbo mwingine kwa wasanii wa Nigeria kumshirikisha Vanessa Mdee ambapo kazi nyingine ambayo Vanessa ameshirikishwa na Legendury Beatz katika ngoma ya ‘Duasi’ iliyoachiwa mwezi Marchi mwaka huu.

Ngoma hiyo ya Move ni ngoma iliyokamilisha idadi ya ngoma 21 zilizopo katika Album ya Reekado ‘Sportligh’ yenye ngoma kama ‘Ladies and Gentlemen’, ‘Oluwa Ni’ feat. Sarkodie ‘Biggy Man’ feat. Falz na nyinginezo nyingi iliyotoka mwezi Septemba mwaka jana.

Hata hivyo Vanessa graph yake kimuziki inazidi kupanda kwakuwa mashabiki wake bado wanangoja ushirikiano mwingine mkubwa na kundi la watayarishaji na Madj, Major Lazer lenye makazi yake nchini Marekani kwakuwa tayari wameshashoot video ya wimbo wao wa pamoja.

 

Comments

comments

You may also like ...