Header

Penny awakataa wasanii wanaomuomba awa-Manage

Mwanamitindo na Mtangazaji wa Tv Penny Mungilwa ambaye alipata umaarufu zaidi kupitia kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii wa muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz amezungumzia suala la kuwasimamia wasanii wa muziki na kulitaja kama jambo lenye ugumu wake.

Akipiga stori na Dizzim Online Penny amesema anatamani sana kuwasimamia wasanii lakini ni kitu ambacho kipo nje ya uwezo wake.

“muziki si kitu rahisi kama watu wanavyofikiria. Unahitaji vitu vingi sana vile vile mimi nina ratiba zangu ambao ziko tight sana na muda wa kuwasimamia mtu itakuwa shida, nitam-let down na wapo wanaonitumia kazi zao nasikiliza ila sina namna”

Hata hivyo mbali na Penny kuliona jambo hilo kuwa na ugumu wake wapo baadhi ya mastaa wa kike waliojihusisha na kuwasimamia wasanii ambao ni pamoja Wema Sepetu, Rose Ndauka na wengine.

Comments

comments

You may also like ...