Header

Simba kuelekea FIFA kudai point tatu za Kagera

Uongozi wa klabu ya soka ya Simba umekiri kupokea barua kutoka bodi ya ligi ambayo imewafahamisha kuhusu kupokonywa alama tatu na mabao matatu kama ilivyoamuliwa na kamati ya sheria, katiba na hadhi za wachezaji ya TFF.

Makamu wa Rais wa klabu ya Simba Jofrey Nyange Kaburu, amesema barua hiyo imewakanganya kama ilivyo kwa wadau wengi wa soka waliopata nafasi ya kuisoma, hivyo wanaendelea na harakati zao za kwenda kuisaka haki shirikisho la mpira Duniani FIFA pamoja na mahakama inayohusika na hadhi pamoja na sheria za wachezaji, CAS.

Hata hivyo Kaburu amesema wanakwenda FIFA kwa lengo la kutaka ufafanuzi wa kina wa kisheria baada ya kuona baadhi ya mambo yamekua yakishindwa kutolewa hukumu na TFF kwa makusudi ya kuwabeba wachache.

Makamu huyo wa Raisi ameongeza kuwa kama ikitokea wanashindwa kupata alama tatu na mabao matatu wanayoyadai dhidi ta Kagera Sugar, bado wana uhakika wa kutatuliwa mlalamiko yao mengine ambayo waliwahi kuyafikisha TFF na kushindwa kupatiwa ufumbuzi wa kisheria na kikanuni.

Simba imefikia hatua hiyo baada ya kupokonywa alama tatu walizopewa na kamati ya masaa 72 hapo awali kabla ya kamati ya sheria, hadhi na katiba kuzirudisha kwa Kagera Sugar, maamuzi ambayo Simba hawajayaridhia.

Comments

comments

You may also like ...