Header

Waziri Mwakyembe awatumia Ali Kiba, Diamond Platnumz, Jose Chameleon, Davido na kutenganisha muziki wa Tanzania na Siasa.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe auzungumzia mwenendo wa wasanii baadhi Tanzania kuhusisha siasa na muziki wao kama njia ya kufikia mafanikio.

Akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na wabunge wakati wa kujadili hotuba ya wabeji ya wizara yake Dkt. Mwakyembe amesema kuwa kila msanii anayo nafasi ya kufanya kazi katika misingi ya sanaa bila jihusisha na masuala ya kisiasa kwakuwa ni kwa asilimia ndogo sana msanii kuweza kupata mafanikio endapo atachukua uelekeo wa siasa.

“mimi nawaomba vijana wangu wanisikilize nimewaambia wanipe mfano wa mwanamuziki yeyote duniani ambaye amefanikiwa kwa kutukana viogozi. Mimi nimeenda Nigeria, Psquare, wasikilize wakina Tiwa Savage, wasikilize wakina Davido, wakina Don Jazzy vijana ambao wengine wamenunua mpaka ndege…very successful lakini nimewaambia ulishwahi kusikia Ohooo Mr. President…” alisema Waziri Mwakyembe.

Aliongeza “Imba nyimbo ambazo zinaweza zikakuletea mafanikio mwenyewe kama unataka siasa kagombee udiwani huko, kagombee nafasi yoyote huko hii ni Entertainment Industry sio Political Industry. Wakina Chameleone, kuna wimbo wowote Chameleone anaongelea serikali ya Uganda, nani successful musician hapa anafanya hivyo?!…”

Hata hivyo Dkt Mwakyembe amehaidi kutoa ushirikiano kwa wasanii bila kujali ukubwa na udogo wa msanii kwa lengo la kufikia mafanikio yao hata kukanusha taarifa za kuwapuuza na wanatelekezwa wasanii mara baada ya kuwatumia kisiasa.

Comments

comments

You may also like ...