Header

Moni Central Zone asimulia alivyo sali sala zake za mwisho

Rapa wa muziki wa kizazi kipya aliyehusika katika tukio la utekaji mwezi uliopita na msanii mwenzake Roma, Moni Central Zone kwa mara ya kwanza amesimulia kilichotokea katika tukio la utekaji.

Akisimuliza kilichotokea Moni amesema kuwa siku ya tukio alikuja mtu aliyemuita Roma nje kwa madai kuwa anahitajika ambapo tukio liliendelea kwa watu wasiojulikana kuingia kwa vitisho studio wakihitaji simu simu ya Roma huku wakilazimisha ampigie simu J-Murder kisha wakachukua simu na kuanza kutumia maneno ya ulaghai ya kuwa walitaka huduma ya studio kama wasanii.

“Yule jamaa wakati ananiambia nimpe simu ya Roma, wakati naifata simu ya Roma akawa ameshaingia akaiwahi akaichukua akaniambia wewe ndo Moni?!…wewe ndo sembe sembe dona??… kaa hapo chini, nimekwambia kaa kwenye kochi simu yako iko wapi?… nikamwambia simu yangu iko kwenye chaji…akamuuliza na Bin Laden? Naye Bin Laden akatoa simu, akauliza Junior yuko wapi?? Mpigie J-Murder…sasa ile hali ya vitisho ikawa imeshaanza.

Kumpigia J-Murder hata kabla sijamaliza maelezo yaani ile Boss kuna watu wamekuja hapa studio, jamaa akanipora simu…oya inakuwaje J-Murder…ohooo sisi hapa tunataka kurecord…tunataka kurecord nyimbo sita…” Alisimuliza Moni Central Zone kupitia XXL ya Clouds Fm

Wakiwa katika hofu na uoga wa kutojua nini kinaendelea Moni na mwenzake Bin Laden hatua za kuwachukua kutoka katika eneo la studio huku wakiamrishwa kubeba vitu baadhi vya studio mpaka lilipokuwa gari, walimkuta Roma akiwa kwenye gari wakingoja waingie na kuondoka nao. Hali ya utekaji iliendelea kwa mateso huku wakiulizwa maswali ambayo hawakuwa na majibu yake kiasi cha kuona kama mwisho wa maisha umefika.

“Muda ambao nakumbuka nimesali sala yangu za mwisho ni ule pale, nikaona dah basi kama kuna kitu nimefanya au kuna kitu nimekosea basi ni kumuachia Mungu” Aliongeza Moni Central Zone.

Hata hivyo tukio lile lililoanza katika sura ya vitisho kisha safari ya kuelekea eneo ambalo waliwekwa kwa kipindi chote cha utekaji liliambatana na kuvulivuliwa mashati kisha kufungwa mikono na macho bila mazungumzo kisha mwendo wa safari ya dakika 40 katika hali ya ukimya mpaka siku ya kutolewa na kutupwa eneo la ambalo waliweza kukiona kiwanda kikubwa na maarufu kilichopo eneo la Tegeta.

Comments

comments

You may also like ...