Header

Nikiona picha za August Alsina nachanganyikiwa, namzimia mpaka basi – Shilole

Shilole amekiri kuwa August Alsina ndiye mwanaume wake wa ndoto.

“Nikionaga picha zake nachanganyikiwa,” amesema muimbaji huyo kwenye kipindi cha Chill na Sky kitakachoruka Jumamosi hii saa nane mchana kupitia Dizzim Online.

“Yaani nachanyikiwa kabisa, nikisikia ana mchumba mimi naumia. Nampenda tu yaani, msela sana sababu mimi mwenyewe msela. [Nimeanza kumpenda] tangu namuona kwenye picha zake na mambo yake yalivyo ya kiselasela, naona kama anaendana na mimi yaani, namuona mnyamwezi halafu ananyuka huyo,” amesisitiza Shishi.

Usikose kusikiliza Chill na Sky Jumamosi hii kumsikia Shishi alivyofunguka vitu exclusive.

Comments

comments

You may also like ...