Header

Bow Wow azungumzia kashfa ya kudanganya kusafiri na private jet

Baada ya kutaniwa vikali mtandaoni kutokana na kudanganya kuwa anasafiri na private jet kumbe anatumia ndege ya abiria, rapper Bow Wow amezungumza.

Jumatatu hii Shad Moss alidai kuwa alipanda ndege binafsi kuzunguka Marekani kufanya promotion ya kipindi chake cha TV, Growing Up Hip-Hop: Atlanta, lakini alipigwa picha akiwa ndani ya ndege za kawaida na kusababisha kutrend kwa hashtag ya #BowWowChallenge.

Alhamis hii, Bow Wow alielezea jambo hilo kwenye mahojiano na kituo cha redio cha Hot 97 kwenye kipindi chao, Ebro in the Morning. “I love it. People don’t understand the scientific method to my madness. Number one, I’m about to have the biggest show on WE tv period…There’s a scientific method to my madness. You gotta just watch the show. Everything is for the show. You gotta just watch the show,” alisema rapper huyo.

Hata hivyo aliongeza kuwa hana tatizo kupanda ndege ya “If I’m going commercial, [it’s] first class always. If I do fly commercial, there’s only three airlines that I do fly: [JetBlue, American Airlines, Delta]. Bang. And I’m flying commercial home today.”

Comments

comments

You may also like ...