Header

Hussein Machozi atangaza wazi kutembeza kichapo

Msanii wa muziki bongo fleva na mmiliki wa ngoma mpya ‘Nipe Sikuachi’ Hussein Machozi amekuwa na mtazamo wa tofauti endapo shabiki wa muziki atakayekuwa na nia ya kutoa maoni hasa kupitia mitandao ya kijamii kuelekea kwake kwa kutumia maneno ambayo atahisi analenga kumvunjia heshima.

Akizungumzia matumizi, faida na umuhimu wa kuwa na matabaka ya timu za wasanii katika muziki wa bongo fleva Hussein Machozi amesema kuwa ni jambo zuri kwakuwa utimu unaleta changamoto na kuchangamsha hali ya ushindani kimuziki. Upande wake Hussein amesema kuwa hana ubavu wa kuendesha muziki wake kwa nguvu ya timu na kuonya kuwa atawatafuta na kuwatembezea kichapo watakao jihusisha na maneno ya maudhi kiasi kilichopitikiza juu yake.

“mimi pia naweza nikafanya timu lakini mimi sina roho hiyo, wenyewe wana roho ngumu sana. Mimi sina timu, mi sipendi matusi…mimi ukinitukana nakufata nakupa vitasa kwasababu sipendi matusi kwa hiyo na timu hizo unaona wanavyomtukana Kiba…wewe mwenyewe unaona mi nitakutafuta kwa mtandao lazima nikupate” Alisema Hussein Machozi alipokuwa akizungumza na ENewz ya EaTv.

Hata hivyo Hussein amemshukuru sana mtayarishaji aliyeshiriki kwenye ngoma yake mpya Man Walter kwa kuwa mshauri mzuri kutokana na mambo kadhaa ambayo yaliendelea mitandaoni yakimlenga kiasi cha kusumbuka kimawazo kwa kuwa ameshiriki kwa kiasi kikubwa kumtulia.

Comments

comments

You may also like ...