Header

Jay Z asaini mkataba mpya wa $200m na Live Nation

Jay Z amesaini mkataba mpya wa miaka 10 wa ziara na kampuni ya Live Nation wenye thamani ya dola milioni 200. Deal hilo litahusisha Live Nation kuandaa na kupromote matamasha yajayo ya Hov kwa kipindi cha miaka 10 ijayo.

Mkataba huo unamaanisha kuwa Jay Z atakuwa akifanya ziara na kampuni hiyo hadi akiwa na umri wa miaka 57.

Hivi karibuni rapper huyo wa pili kwa utajiri duniani (baada ya Diddy), amepunguza idadi ya show na kujikita kwenye biashara zingine, lakini kwa mkataba huu inamaanisha kuwa atarudisha kasi yake.

Comments

comments

You may also like ...