Header

Mambo 11 ya kufahamu kuhusu bondia Anthony Joshua

Haya ni Mambo 13 ya kufahamu kuhusu bondia Anthony Joshua

1. Aliingiza £15m kwenye pambano lake na Wladimir Klitschko ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 43.

2. Anaishi na mama yake, Yeta Odusanya aliyehamia Uingereza toka Nigeria miaka ya 80. Baba yake ni nusu Mnaijeria na nusu Muarish

3. Hamruhusu mama yake kuangalia mapambano yake, iwe live ulingoni ama kwenye runinga

4. Pamoja na umaarufu wake, awapo nyumbani hufanya kazi za kawaida kama kijana wa kawaida
“Kitu pekee ambacho namuomba mama yangu anisaidie ni chakula changu, kwahiyo hufanya zaidi shopping, kununua samaki, nyama, kuku na vingine,” alisema kwenye interview moja.

5. Ana kipaji cha kucheza soka na aliwahi kufanyiwa majaribio kwenye klabu ya Charlton Athletic

6. Mwaka 2011, alikamatwa na polisi akiendesha gari kwa mwendo kasi na kukutwa na mfuko wa bangi kwenye kiti cha abiria. Tukio hilo lilimfanya aache kutumia kilevi cha aina yoyote

7. Ameshinda mapambano yake yote 19 aliyowahi kupigana na yote ni kwa knockout

8. Ni mkurugenzi wa makampuni sababu, likiwemo la nyumba, magari na masoko
9. Scott Welch, bingwa wa zamani wa ndondi wa Uingereza anaamini kuwa Joshua anaweza kuja kuwa mwanamasumbwi bilionea wa kwanza duniani

10. Ni msomaji sana wa vitabu hasa vya biashara na anapenda kucheza chess baada ya kushawishiwa na Lennox Lewis

11. Ana mtoto wa kiume, Joseph aliyezaliwa Oct, 2015 na aliyezaa na ex wake, Nicole Osbourne, anayefanya kazi kama mwalimu wa dance

Comments

comments

You may also like ...