Header

Wema Sepetu ayamaliza kwa kuparty na Diamond Platnumz pamoja na Sallam Sk

Muigizaji na staa wa bongo movie Wema Sepetu amebadilisha mategemeo ya wengi walioshiriki party ya meneja wa msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz ‘Sallam Sk’ usiku wa jana baada ya kutoka kizamani zamani na nakusherehekea kwa pamoja na wote waliofika.

Akizungumzia furaha yake ya kushiriki party hiyo iliyopewa maudhui ya miaka ya 90(90s) Wema amesema kuwa kwake haoni sababu ya watu kuona kuwa hasingefika kwakuwa hayuko tena katika mahusiano na Diamond Platnumz na kusema kuwa hakuna sababu za kuendelea kuishi maisha ya kutoelewana siku zote.

“kwanini hawakutegemea??!…walikuwa wanategemea kwamba mabifu yaendelee mpaka mwisho wa maisha yetu??” Alisema Wema Sepetu alipkuwa akiongea na Ayo Tv..

 

Hata hivyo Wema alimtakia maisha mema meneja Sallam Sk na kumtaja kuwa mbali na urafiki wao amemfahamu zaidi kama mtu anayetumia muda wake sana kwa ku-party kila anapokuja katika mfumo wake wa maisha na mambo ya kula good time hata kumuita ‘Party animal’.

Comments

comments

You may also like ...