Header

Antonio Conte amwaga shukrani kwa Mashabiki na Wachezaji

Meneja wa Chelsea Antonio Conte ameelekeza shukrani zake za dhati kwa wachezaji wake baada ya kutwaa taji la Ligi Kuu Uingereza 2016-17 kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya West Bromwich Albion.

Muitaliano huyo ameelezea ushindi huo kama “mafanikio makubwa” na ameshukuru umoja baina yao na mashabiki, kampeni za kukumbukwa katika Stamford Bridge.

Asanteni, asanteni. Haya ni mafanikio makubwa kwa wachezaji. Nawashukuru sana kwa mafanikio na kazi njema waliyofanya. Wamenionyesha moyo wa kujituma na kujitahidi kupata mafanikio makubwa msimu huu. Baada ya ushindi huu ni lazima tuwe na furaha, tumefurahi sana.Alisema Conte

Michy Batshuayi akitokea benchi alikuwa shujaa wa Chelsea kwa kufunga goli ambalo liliwazamisha West Brom na kutwaa taji dakika ya 82.

Comments

comments

You may also like ...