Header

Azam Fc wamzuia Kapombe kutimkia Msimbazi

Azam FC imezima ndoto za Simba kumrejesha beki wao wa zamani, Shomari Kapombe, baada ya kuingia naye mkataba wa awali hatua hiyo ya klabu ya Azam ni kama imevuruga mipango ya klabu ya Simba.

Akizungumza na gazeti la Bingwa Meneja wa Azam FC, Philipo Alando, alisema klabu hiyo ilikaa na Kapombe wiki mbili zilizopita na kujadiliana naye kuhusu hatima ya mkataba wake baada ya huu wa sasa kumalizika na kukubaliana kuingia naye mkataba mwingine wa awali wa miaka miwili.

“Katika kikao chetu na Kapombe, kikubwa aliomba aboreshewe vitu  muhimu pamoja na kutupa taarifa ya ofa aliyoipata ya kwenda kucheza nje. Alisema Alando

Kabla ya kutua Azam misimu miwili iliyopita, Kapombe aliichezea Simba kwa mafanikio makubwa yaliyomwezesha kuivutia klabu ya AS Canes ya Ufaransa, ambayo ilimsajili kabla ya kuachana nayo na kujiunga na Azam FC.

Comments

comments

You may also like ...