Header

Harmonize atembelea wangonjwa hospitali ya mkoa Mtwara

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka lebo ya muziki ya WCB ‘Harmonize’ pamoja na timu yake kwa pamoja wametembelea wagonjwa katika Hospitali ya mkoa ya Ligula iliyopo Mtwara huku akipewa ushirikiano na Youngkiller Msodoki na Shilole miongoni mwa wasanii waliomsindikiza katika ziara yake iliyopewa jina ‘Harmo Night Tour’ iliyoanzia mkoani Mtwara.

Akizungumza na Dizzim Online Harmonize amesema kuwa katika ziara yake mkoani Mtwara wapo wenye afya njema ambao baadhi yao wana uwezo wakufika katika shows zake lakini wakati huo huo wapo ambao pengine wanatamani kushiriki kuona matumbuizo yake lakini kutokana na afya zao kutokuwa njema wanaishia kuugulia na kuitaja kama moja ya sababu iliyomsukuma kufika kuwaona na kuwajulia hali wagonjwa hospitalini hapo.

Hata hivyo Harmonize kwa kushirikiana na uongozi mzima wa WCB ametoa kipaumbele katika mkoa huo wa Mtwara ambao jana alitumubiza katika viwanja vya Polisi Mess Zaman Makonde Beach, leo atatumbuiza Masasi katika viwanja vya Emirates Hall kisha kesho Nachingwea katika viwanja vya Nachingwea Resorts ambapo kwenye muendelezo wa ziara hiyo inatazamiwa kuzunguka mikoa mingi ya Tanzania.

Comments

comments

You may also like ...