Header

Mfungaji bora anatokea Yanga-” Tambwe”

Mshambuliaji wa Yanga na Timu ya Taifa ya Burundi Amiss Tambwe amesema kwa jinsi mambo yanavyokwenda, ana uhakika asilimia 100 mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara atatokea katika timu yake.

Mshambuliaji huyo anapta jeuri ya kusema hayo kutokana na ukweli kwamba, katika kikosi chao ndipo wanapotokea wachezaji wengi wanaojua kufunga.

“Hadi hivi sasa ni uhakika kuwa mfungaji bora wa msimu huu anatoka Yanga, hili halina ubishi na wala halihitaji kubishana na mtu, kikubwa kama kuna ambaye anaweza kubisha asuburie hadi mwisho tuone. Alisema Tambwe.

katika kufanikisha hilo wanamtoa mfungaji bora, wamepanga kucheza mechi zote zilizobakia kwa ushirikiano bila ya kunyimana pasi kwenye safu yao ya ushambulia alimalizia kwa kusema hayo Tambwe.

Comments

comments

You may also like ...