Header

Novak Djokovic atembeza kichapo bila Kocha huko Madrid

Novak Djokovic ameshinda mechi yake ya kwanza Madrid Open dhidi ya Nicolas Almagro juzi Jumatano, tangu athibitishe kuondoka kwa makocha wake.

Mcheza tenisi huyo namba 2 duniani alishinda kwa seti mbili (6-1 4-6 7-5) katika raundi ya kwanza ya michuano hiyo, ikiwa ni muda mfupi tangu atangaze kuwa amemtimua kocha wake, Marian Vajda

Nahitaji kufikiri kujua nani namhitaji kuwa kocha wangu. Kwa sasa niko mwenyewe bila ya kocha, lakini nafikiri wakati wa michuano ya French Open au baada ya French Open I (mimi) nitakuwa nimeshapata kocha“Alisema Novak.

Katika mchezo wake mwingine atakutana na mchezaji mwingine wa Hispania, Feliciano Lopez, katika hatua ya 16 bora.

Comments

comments

You may also like ...