Header

Mmiliki wa Facebook ‘Mark Zuckerberg’ atimiza umri wa miaka 33

Ni siku kubwa sana duniani ambapo walio wengi wa wanasherehekea siku ya mama duniani(Mother’s Day) pia ni siku ya mfanano wa tarehe ambayo amezaliwa mkurugenzi na mwanzilishi wa mtandao wa Facebook Mark Elliot Zuckerberg.

Mark Zuckerberg amezaliwa wa 1984 na mpaka sasa anamiliki mali zenye tahamani ya dola za kimarekani billioni 62.6 ambapo mwanzoni mwa mwaka huu kwa mujibu wa jarida la Forbes aliingia katika orodha ya matajiri 10 duniani na kushika nafasi ya 5 orodha iliyoongozwa na Billionea ‘Bill Gates’ katika nafasi ya kwanza.

Moja ya mambo ambayo mmiliki huyu wa mtandao wa facebook yanawashangaza wengi ni kutoamini katika mungu hata kuwa miongozi mwa matajiri duniani wanaongoza kwa mfumo mbaya wa mavazi tofauti na ukubwa pamoja na heshima anayopewa na wanaotambua nafasi yake duniani hasa katika ulimwengo wa mitandao ya kijamii.

Hata hivyo mbali na kuwa anamiliki mtandao wa facebook pia ni mmiliki wa mitandao mingine maarufu kwa matumizi ya mawasiliano na mitindo ya maisha ambayo ni pamoja na WhatsApp na Instagram na katika siku ya leo anasherekea pamoja na mwana miweleka maarufu Zack Ryder na muongozaji wa filamu maarfu George Lucas.

Comments

comments

You may also like ...