Header

Mtoto wa Brenda Fassie, Bongani afulia licha ya kurithi mamilioni ya mamaye

Mtoto wa kiume wa marehemu Brenda Fassie, Bongani Fassie, ambaye wiki hii alijigamba kuwa ni tajiri baada ya kurithi mali za mama yake zifikazo rand milioni 20 (shilingi bilioni 3.4), yuko mbioni kutumuliwa kwenye nyumba aliyopanga jijini Johannesburg baada ya kushindwa kulipa kodi kwa miezi mitatu sasa.

Bongani, msanii wa hip hop aliyekuwa member wa kundi la Jozi, amepewa muda hadi mwisho wa mwezi huu kuitafuta kodi hiyo, lasivyo anatimuliwa, kwa mujibu wa gazeti la Sunday World la nchini humo.

Fassie anadaiwa R34000 baada ya kushindwa kulipa kodi yake ya R1300 (shilingi 221,00 za Kitanzania) kwa usiku mmoja kwenye apartment hiyo.

Comments

comments

You may also like ...