Header

One Africa Music Fest: Jidenna ashindwa kutumbuiza baada ya muda kuisha na umeme kukatwa

Staa wa Classic Man, Jidenna usiku wa kuamkia leo alishindwa kutumbuiza kwenye tamasha la One Africa Music Festival baada ya muda kuisha na umeme kukatwa na waendeshaji wa ukumbi wa SSE Arena, Wembley, London.

Kutokana na muda kutokuwa upande wa waandaji, waliongezwa dakika 20 kumaliza show lakini bado walishindwa kuutumia muda kwa kutumia nusu yake kuandaa show inayofuata ambapo Flavour na Psquare walipanda. Wakiwa jukwaani kutumbuiza, umeme ndani ya ukumbi huo ukakatwa.

Hali hiyo iliwanyong’onyeza wahudhuriaji wa show hiyo walioanza kuondoka na kuahidiwa afterparty. Kukatwa kwa umeme kulimwathiri Jidenna, ambaye hakuweza kutumbuiza kutokana na waandaji kushindwa kutumia muda vizuri.

Kupitia Instagram, Jidenna aliandika:

Cheers to the artists and organizers of #OneAfrica! I was supposed to perform 2night but the show was cut off as I waited backstage. I’m disappointed that London wasn’t able to see me 2night. Regardless of whose to blame, to make this our time we must be on time #OneAfrica

Wasanii wengine waliotumbuiza usiku wa jana ni pamoja na Alikiba, Tekno, Sarkidie, M.I, Awilo Longomba, Davido, Tiwa Savage, Banky W, Victoria Kimani na wengine.

Comments

comments

You may also like ...