Header

Ripoti: Baada ya Tyga, Kylie Jenner azama rasmi kwenye penzi la rapper huyu

Ukurasa wa uhusiano kati ya Tyga na mrembo na staa wa Instagram, Kylie Jenner umefungwa rasmi. Ni kwa sababu Kylie amezama kwenye penzi na rapper Travis Scott. Kwa mujibu wa TMZ, uhusiano wao ni rasmi kabisa sasa.

Vyanzo vimeiambia website hiyo kuwa wawili hao hawaachani tangu wajumuike pamoja kwenye tamasha la Coachella hivi karibuni, na sasa wameamua kuanzisha uhusiano rasmi. Mtandao huo umesema mrembo huyo ameanza kuwa karibu na rapper huyo kwa kumfuata kwenye mji anaoshi, Houston.

Pia Kylie ameshakutana na familia ya rapper huyo. Wamekuwa wakizunguka pamoja kuanzia Miami, kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Travis, NYC, LA na H-town. Kwa sasa uhusiano wao upo katika hatua ya furaha zaidi.

Comments

comments

You may also like ...