Header

Simon Msuva achanika juu Jicho

Simon Msuva ambaye jana aliipatia Yanga goli la kwanza mnamo dakika ya 7 ya pambano hilo dhidi ya Mbeya City, mfungaji huyo aliumia na kupelekea kutoka mchezoni.

Taarifa kutoka kwa madaktari wa Yanga inasema kuwa mchezaji huyo ameumia sehemu ya juu ya uso wake baada ya kuchanika na kushonwa nyuzi nne.

“Saimon Msuva amechanika juu ya jicho lake la kushoto ambapo ameshonwa nyuzi nne baada ya kugongana na mchezaji wa Mbeya city wakati akifunga goli lake la 14 kwenye ligi kuu Tanzania bara msimu huu” Alisema Daktari Huyo.

Msuva ambaye msimu huu amekuwa kwenye kiwango bora na mpaka sasa akifunga magoli 14.

Comments

comments

You may also like ...