Header

Jinamizi la Majeruhui laitembelea Serengeti Boys

Nahodha wa timu ya Serengeti Boys, Issa Abdi Makamba ameondolewa kwenye Kikosi kinachotarajiwa kushuka leo dimbani kuvaana na Mali katika michuano ya AFCON U-17 huko Libreville nchini Gabon baada ya kupata mpasuko wa mguu wakati akifanya mazoezi.
Hayo yamebainishwa na Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime na kusema ni jambo la kusikitisha kwa kumkosa Nahodha huyo katika michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 katika hatua ya makundi kutokana na majeruhi aliyoyapata wakati akishirikiana mazoezi na wenzake

Ni jambo la kusikitisha kidogo kwamba Nahodha wetu Issa Abdi Makamba alipata mpasuko wa mguu juzi mazoezini kwa bahati mbaya akiwa pekee yake kabisa…Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa madaktari wangu wamesema kwamba hatoweza kushiriki mashindano haya” Alisema Shime

Serengeti Boys itaushika Dimbani leo kuchanga karata yake ya kwanza dhidi ya Mali majira ya Saa 11;30 kwa saa za Afrika Mashariki.

Comments

comments

You may also like ...