Header

Katy Perry mbioni kuwa jaji mpya wa shindano la American Idol

Katy Perry yupo ukingoni kufunga makubaliano ya kuwa jaji mpya wa shindano la kuimba la American Idol na huenda akatangazwa rasmi kesho, kwa mujibu wa TMZ. Bado haijaulikana majaji wengine wawili watakuwa akina nani. Kwa upande wa host, Ryan Seacrest anatarajiwa kurejea tena.

Shindano hilo lilisimama kuruka kwa muda kupitia kituo cha FOX na sasa litarejea kupitia kituo cha ABC. Hata hivyo inadaiwa kuwa majaji wengine wawili hawatakuwa watu wenye majina makubwa ili kupunguza gharama za kuwalipa.

Shindano pinzani, The Voice la NBC, limewasaini washiriki wa zamani wa Idol, Jennifer Hudson na Kelly Clarkson kama makocha wa msimu mpya. Pia Katy amewahi kutosa ofa za mwanzo za kujiunga na Idol, wakati ilipokuwa ikiruka kwenye kituo cha runinga cha Fox.

Comments

comments

You may also like ...